ABNA inatuarifu kua; Maoni tofauti yametolewa na jumuiya za kimataifa kuhusu kuongezwa kwa hadhi ya Palestina kwenye Umoja wa Mataifa. Mkutano 67 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa umepitisha azimio la kuongeza hadhi ya Palestina kwenye Umoja huo kuwa mjumbe mwangalizi. Nchi wanachama 138 walipiga kura za ndiyo, huku nchi 9 zikiongozwa na Israel na Marekani zikipiga kura ya hapana, nchi nyingine 41 hazikupiga kura hiyo.
Aidha ushindi huo ulisababisha ghadhabu za ujumbe wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Susan Rice, kumesema: Wananchi wa Palestina watagundua kuwa, mambo machache sana yamebadilika, na matarajio ya amani ya kudumu yamezidi kupotea. Pia Balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa Ron Prosor alisema: Azimio hilo ni ujumbe kuwa Jumuiya ya kimataifa iko radhi kufumbia macho makubaliano ya amani.
Kwa upande mwengine Rais Francois Hollande wa Ufaransa ametoa taarifa ya kuipongeza Palestina ikisema, kura hiyo inaendana na ahadi ya Hollande ya kuunga mkono kutambulika kwa taifa la Palestina kimataifa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hong Lei amesema: kufanikiwa kwa Palestina kuwa nchi mwangalizi katika Umoja wa Mataifa ni maendeleo mengine makubwa kwa Palestina katika njia yake ya kuanzisha nchi kwa kujiamulia, na China inakubali kwamba kuanzisha nchi kwa kujiamulia ni haki halali ya wananchi wa Palestina